Malumbano ni hasa upande wa viongozi wa Jumuia ya kiislamu nchini Burundi COMIBU : kuna kundi la sheikh Sadik Kajandi anayetambuliwa na wizara ya mambo ya ndani na kundi la Al-Haj Haruna Nkunduwiga aliyeteuliwa na baraza kuu la mashehe.
<doc1909|right>« Allah Akbar, Allah Akbar, Allah Akbar, Mwenyezi Mungu ni mkubwa », bada ya takbira hizo na bada ya Imam aliyeongoza swala kutowa hutba yake akiwaomba waislamu kushikamana, Sheikh Sadiki Kajandi, anayezidi kubaini kuwa ndie kiongozi wa Jumuia ya kiislamu nchini Burundi alitolea wito waislamu akiwataka kuzidi kupendana, na kuombea Burundi ipate usalama. Aliwaomba pia kutotega sikio ’’wale wanaotaka kusambaratisha waislamu’’. Kundi hilo aliliomba kutoendelea katika njia hio ’’sababu uislamu ni amani’’. Wapinzani wake hao aliwaomba wasiendeleye kuleta mfarakano na shari baina waislamu. Sheikh Kajandi alionekana akiwa na kundi la watu waliokuwa wakimfuata kwa karibu, ’’pengine ni walinzi wake’’, alisema hayo muumini mmoja bada ya ibada hio.
Ibada yenyewe ilifanyika chini ya ulinzi mkali, kwenye uanja wa COMIBU tarafani Nyakabiga. Kilicho dhahiri ni kua idadi ya askari polisi iliongezwa ikilinganishwa na miaka iliyopita. Kawaida, badhi ya waislamu jijini Bujumpbura hua wanapenda kujumuika kwenye uanja huo wa COMIBU licha ya kua ibada zilifanyika katika tarafa zingine za mji wa Bujumbura kama huko Kibenga tarafani Kinindo, Kanyosha, Buyenzi na Buterere.
Licha ya kua uanja wa Nyakabiga uliandaliwa na Al-Hajj Haruna Nkunduwiga Kiongozi wa jumuia ya kiislamu nchini Burundi, aliyeteuliwa na Baraza kuu la mashehe, akiambatana na waislamu zaidi ya 200, kiongozi huyo wa COMIBU ambae bado kutambuliwa na wizara ya mambo ya ndani na kundi lake walichukuwa uamzi wa kisalia tarafani Buterere. « Uamzi huo umechukuliwa ili kusitokeye vurugu wakati wa ibada sababu ilionekana Kajandi alikuwa na wahuni karibu kumi ambao walikuwa tayari kuvuruga sala walakin hatukuwapa na fursa hio sababu uislamu si diniya mvutano ».
<doc1908|left>Al-Hajj Nkunduwiga anapongeza waislamu kwa kudiriki sala katika hali ya utulivu. Alimtolea wito waziri wa mambo ya ndani aheshimishe sheria kwa kuwatambua viongozi walioteuliwa na waislamu na ’’ikiwa Bw. Kajandi ana sifa fulani ambazo zinamridhisha waziri huyo basi ampe kazi’’, anazidi kusema kiongozi huyo wa Jumuia ya kiislamu nchini Burundi aliyeteuliwa na Baraza kuu la mashehe.