Wafuasi hao 5 wa Agathon Rwasa, kinara wa zamani wa chama cha waasi cha FNL ambae wakati huu yiko mafichoni walichukua uamzi huoa wa kuomba hifadhi kwenye ofisi za Halmashahuri Huru ya Haki za Binadamu kwa kuhofia usalama wao. Wanaomba wafamishiwe katika nchi nyingine. Kiongozi wa Halmashahuri hio anaahidi kutanzuwa swala hilo.
Vijana hao kutoka wilayani Kanyosha , mkoa wa Bujumbura wakati huu wana muda wa zaidi ya awiki moja wakiishi kwenye ofisi za Halmashahuri hio. Wanabaini kua walichukuwa uamzi wa kukimbia bada ya kutishiwa kumaliziwa maisha na hapa wanasuta kidole askari polisi, idaraza upelelezi na vijana wakereketwa kutoka chama tawala cha CNDD FDD.
’’Wanataka kutufyeka’’, anasema kwa sauti ya kutetemeka moja kati ya wafasi hao wa Agathon Rwasa, kinara wa chama cha zamani cha waasi cha FNL ambae wakati huu aliengia mafichoni bada ya madai ya uizi wa kura kwenye chaguzi za hapo mwaka jana zilizopelekea chama cha CNDD FDD kujipatia ushindi.
’’Hata kwenye ofisi za Halmashahuri Huru ya Haki za Biadamu hio tulipo kimbilia bado tuna hofu sababu kuna vitisho, tunapigiwa mara kwa mara simu na watu wasiojulikana na jawabu kwetu ni kupelekwa ugenini’’, wanazidi kusema wakimbizi hao wa aina nyingine.
Kwa upande wake kiongozi wa Halmashahuri Huru ya Haki za Biadamu hio, Emmanuel Ntarutimana anasema ana mawasiliyano na idara za upelelezi, utawala hata waakilishi wa vijana wakereketwa wa chama tawala cha CNDD FDD sababu ni miongoni mwa watu wanaopelekea wafuasi hoa wa Agathon Rwasa kupatwa na uoga.
Kiongozi wa Halmashahuri hio anawatuliza wafuasi hao wa Agathon Rwasa, anasema jawabu ni hivi karibuni. Licha ya hayo anakiri kua swala hilo si rahisi huku akiomba kuepo uelewano na kuaminiana. Anatolea wito wafadhili ili wachangie katika kuwahudumia watu hao, anasema Halmashhuri Huru ya Haki za Binadama haikujiandalia hali hio.