Msako ulioanzishwa na polisi kwa ushirikiano na idara ya upelelezi tangu wiki iliyopita umeisha pelekea watu wasiopungua 45 pakiwemo mwandishi wa redio Bonesha FM, Hassan Ruvakuki kutiwa ndani. Msako huo ni hasa katika mikoa ya Muyinga, Ngozi, Karuzi n Cankuzo. Baadhi ya watu hao ni waalimu, na ni wafuasi wa chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa.
<doc2279|left>Kando ya shutma kua watu hao walishiriki katika ’’vitendo vya kigaidi’’, wengine wanashakiwa kua wanashirikiana na ’’kundi lipya la waasi’’ lililozuka huko mkoani Cankuzo mashariki mwa Burundi. Kanali Pierre Claver Kabirigi anadai kuwa kiongozi wa kundi hilo liitwalo FRD-Abanyagihugu.
Mkoa ‘’’unaotia fora’’ ni Muyinga ambapo kulikamatwa watu 18 pakiwemo mwanamke mmoja ambae aliwahi kuwa mbunge wa chama cha Sahwanya-FRODEBU. Katika msako ulioendeshwa kwenye nyumba ya mbunge huyo wa zamani kulikamatwa nyaraka mbalimbali na picha ikimuonesha mama huyo akiwa pamoja na mbunge Kanali Pierre Claver Kabirigi anaedai kuwa kiongozi wa kundi hilo lippya la waasi liitwalo FRD-Abanyagihugu, huku mwandishi wa redio Bonesha FM Hssan Ruvakuki akiwa na maikriphoni akiwahoji. Katika nyaraka hizo kulikamatwa pia orodha ya watu hao wanaoshakiwa kuwa na ushirikiano fulani na Kanali Pierre Claver Kabirigi.
Huko mkoani Ngozi kulikamatwa hio jana walimu 2, wote hao ni wafuasi wa chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa. Mmoja ni kutoka tarafa ya Ruhororo, ni naibu kiongozi wa shu na ni mwanamemba wa halmashahuru ya tarafa hio. Mwengine ni kutoka tarafa ya Mwumba. Mwalimu huyo alikamatwa bila waranti.
Na huko mkoani Karuzi kumeishatiwa nguvuni watu 7, baadhi yao ni waalimu. Wote kwa jumla ni wafuasi wa chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa. Miongoni mwao kuna mwanamke mmoja ambae amekamatwa huku akiwa na mtoto mchanga. Wote hao walikamatwa pasina waranti.
Na huko mkoani Cankuzo mashariki mwa Burundi kumeisha kamatwa watu 9 tangu tarehe 21 mwezi novemba. 8 miongoni mwao ni wafuasi chama cha FNL watiifu wa Agathon Rwasa na mmoja ni kutoka chama cha UPD-Zigamibanga cha upinzani.