Ndege hio ya aina ya Boeing737-800 ambayo imetuwa kwa mara yake ya kwanza kwenye uanja wa ndege wa Bujumbura ni ya kipekee katika eneo la Afrika mashariki. Ina uwezo wa kubeba uzito wa tani 8 pakiwemo abiria 154 na ndege hio italeta manufaa kwa wafanyabiashara wa eneo la Jumuia ya Afrika Mashariki, amesema hayo Patrick Nkulikiyimfura, mwakilishi wa shirika la ndege la Rwanda, Rwandair akiwa pamoja na waziri wa Burundi anayehusika na maswala ya Jumuia ya Afrika Mashariki, Bii Hafsa Mosi. Waziri wa Burundi wa uchukuzi, Saïd Kibeya amebaini kua ndege hio italeta mwamko mpya katika uchukuzi na ni kwa maendeleo ya Burundi na kanda hii ya Afrika ya mashariki, amezidi kusema waziri Saïd Kibeya.