Bada ya hapo alasiri Bw. Fabien Segatwa, wakili mtetezi wa Bw. Léonce Ngendakumana, kiongozi wa chama cha FRODEBU ambae pia ni kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani uitwao ADC-Ikibiri, kubaini kua kuna uwezekano au hatari kinara huyo wa upinzani apelekwe kwenye jela kuu ya Mpimba, mwendeshamashtaka katika manispaa ya jiji la Bujumbura ameamuru mwanasiasa huyo arejee nyumbani. Walakin hayo ni bada ya kukamatwa hapo alfajiri na askari polisi na kupelekwa mahakamani. Si hayo tu, askari polisi hao wameonekana leo hii wakifanya uchunguzi mara mbili kwenye nyumba ya kiongozi huyo wa muungano wa vyama vya upinzani.