Hakimu Rémy Nsabimana aliyesimamia kesi hio alitiwa ndani kwenye jela ya Ngozi hapo ijumapili disemba 6 jioni. Analaumiwa kuibia nyaraka fulani kwenye faili ihusuyo kesi hio ya mauaji ya Sista Manic Lucrezia kutoka Croatia na Francesco Bazzani, raia wa Italy amabao walikuwa wakitowa huduma kwe hospitali ya Kiremba, mkoani Ngozi, kaskazini mwa Burundi. Watuhumiwa ambao ni wanafunzi 2 walikatiwa adhabu ya kifungo cha maisha. <doc2280|left>Hakimu huyo aliwekwa kizuizini bada ya kuhojiwa kwa siku nzima na mwendeshamashaka mkuu kwenye mahakama ya rufaa jijini Ngozi, Jérôme Ndaje. Faili ya hakimu huyo imekwisha funguliwa, ni ’’RMPG 2887/NJ’’. Licha ya hayo hakimu huyo aliyesimamia kesi hio anabaini kua mwendeshmashtaka alimtia ndani sababu alimruhusu, bada ya kesi kukatwa (ni kinyume na sheria), mtuhumiwa mmoja katika mauaji hayo kutowa kauli yake ambapo alikiri kua mauaji hayo njama zilipangwa na viongozi fulani wa ngazi za juu pakiwemo mbunge Jean Baptiste Nzigamasabo maarufu Gihahe. Mwendeshamashaka mkuu kwenye mahakama ya rufaa jijini Ngozi, Jérôme Ndaje anatupilia mbali madai hayo, anasema hali ya kua mtuhumiwa huyo alipewa nafasi ya kijitetea na huku kese iwekwisha malizika haibadili chochote. Duru za kuaminika kutoka Ngozi zasema hakimu huyo hana hatia na hakimu huyo anakiri kua kamwe hakugusa fali hizo. Mwendeshamashaka mkuu kwenye mahakama ya rufaa jijini Ngozi anasema hatosita kufanya uchunguzi mwengine ikionekana wa kua kuna dosari fulani. Kana mashahidi wengine ambao wamesikilizwa hapo ijuma tano tarehe 7 disemba. Duru kutoka Ngozi zasema faili hio inaonekana kufwuatiliwa kwa karibu na afisa wa idara ya upelelezi. Hata hapo ijuma pili afisa hao walionekana wakati mwendeshamashaka mkuu kwenye mahakama ya rufaa jijini Ngozi akimhoji hakimi huyo aliyesimamia kesi ya Mauaji ya raia 2 kutoka Ulaya.