Wafanyabiashara wa Burundi wenye malori bada ya malalamiko yao kua ushuru unaotozwa kwa kuingia nchini Tanzania ni ghali waamua kubadilisha na kupachika pleti namba za Tanzania.
Kwa mujibi wa baadhi ya madereva, wakati huu watu watapumua, heri kua na lori yenye pleti namba ya Tanzania kuliko kua na lori yenye pleti namba ya Burundi sababu ni rahisi kuingia nchini Tanzania hasa upande wa ushuru hakuna tena. Malori yote ya mjini Gitega katikati mwa Burundi yaliisha pachikwa pleti namba ya Tanzania na lengo ni kuingia tanzania bila kutozwa ushuru.
Madereva hao wanabaini kua kila lori yenye pleti namba ya Burundi inatozwa dola za kimarekani 500 kwa kuinngia nchini Tanzania hayo ni wakati malori kutoka Tanzania yanapita bila malipo yoyote. Baadhi ya malori hayo unakutana kwa mwezi yanahesabu safari karibu 10 hali ambayo inapelekea madereva kupoteza pesa nyingi. « Kama lori ina pleti namba ya Tanzania mtu anafaidika. Kwa kila safari unakutana umeweka kando dola za kimarekani 348. Hapo mwaka jana ilinibidi nilipe dola 50,000.
Mambo hayo hayawezi kuendelea, mtu anaweza kufirisika na nilichukua uamzi wa kubadilisha pleti namba », anasema hayo moja kati ya madereva wa malori hayo yanayofanya misafara kuelekea Tanzania. « Upande wa madereva kutoka Tanzania kwenye kituo cha mpakani, forodhani wanatozwa pesa zipatazo dola 152 na bado mtu anajiuliza ni manufaa gani ya kuingia kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki », anasema Ernest Banzubaze, dereva mwengine.
Huo ni ukwepaji kodi
Kwa mujibu wa afisa wa idara ya ushuru forodhani, hakuna sheria yoyote iliokiukwa kutokana na uamzi huo wa kubadili pleti namba. Iwapo wafanyabiashara walichukua uamzi huo pengine kuna urahisi fulani nchini Tanzania. « Walakin wachunguze vizuri, unaweza kukutana raia kutoka ugenini wanatozwa ushuru ambao haulingani na ule unaolipishwa wafanyabiashara wa nyumbani », anazidi kusema afisa huyo.
Kilicho wazi ni kua kiwango cha malori yenye pleti namba kutoka Tanzania kiliongezeka maradufu. Upande wake Pierre-Claver Simbizi kutoka Mamlaka ya Mapato Burundi, OBR, tawi la Gitega katikati mwa Burundi anasema uamzi wa matajiri hao wenye malori wa kubadilisha na kupachika pleti namba za Tanzania ni miongoni mwa ukwepaji kodi. « Na haijulikani iwapo hakuna kasoro kisheria upande wa makaratasi yote yanayohitajika nchini Tanzania kwa malori ya mabosi hao », anazidi kuuliza afisa huyo wa Mamlaka ya Mapato Burundi akiahidi kua uchunguzi utafanyika hivi karibuni ili atakae kutwa na hatia aadhibiwa kwa mujibu wa sheria.