Jeudi 26 décembre 2024

Archives

Mabadiliko ya serekali nchini Burundi

05/05/2013 Commentaires fermés sur Mabadiliko ya serekali nchini Burundi

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, alifanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri hapo ijuma tatu novemba 7, Mawaziri 4 ni wapya katika baraza hilo, mawaziri wengine 6 pakiwemo waziri wa Usalama, Alain Guillaume Bunyoni na waziri wa Mambo ya kigeni, Augustin Nsanze wametolewa madarakani walakin tayari vigogo hao 2 pamoja na mhandisi Saïd Kibeya wameisha pewa nafasi nyingine kwenye ikulu ya rais kama washauri.

Wadadisi wa mambo wanasema kando ya lengo ni kuboresha utawala bora, madhumuni ya mabadiliko hayo ni kuandaa kongamano la chama tawala cha CNDD FDD linalotazamiwa kufanyika hapo mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2012. Wachunguzi wa mambo hao wanasema mabadiliko yaliyokuwa yakianza kufurahiwa kua pengine yataleta muamko mpya yanaonekana hayatoleta matumaini makubwa sababu, kama wasemavyo wadadisi wa mambo hao ’’vigogo ni wale wale tu, wanabadilisha nafasi tu ! ’’

Katika mabadiliko hayo kuna hasa Kamishna wa polisi Gabriel Nizigama ambae anashikilia wakati huu hatamu za uongozi wa wizara ya usalama akichukuwa nafasi ya Alain Guillaume Bunyoni.

Duru za kuaminika zasema kiongozi huyo ambae ni miongoni mwa vigogo wa utawala inatazamiwa achukuwe nafasi ya uongozi wa chama cha CNDD FDD na lengo ni kukomeshwe mvutano kati kiongozi wa chama hicho na katibu wake, na hasa lengo lingine ni kumteuwa kiongozi mwenye ukaribu na Rais wa Jamhuri. Hapo majuzi kwenye kanisa inayoongozwa na mkewe Rais wa Jamhuri kulifanyika sherehe za kumbatiza Alain Guillaume Bunyoni.

Katika mabadiliko mengine muhimi kuna marekebisho kwenye wizara ya mambo ya kigeni ambayo wakati huu inaongozwa na Balozi Laurent Kavakure akichukuwa nafasi ya Augustin Nsanze ambae alikuwa ziarani Teheran. Duru zasema baadhi ya wafadhili wa Burundi watapumua sababu walikuwa wakiomba waziri huyo atolewe madarakani akishtumiwa kua alisababisha uhusiano baina Burundi na wahisani wake kuzorota.

Upande wake waziri mpya huyo Laurent Kavakure bada ya kuiwakilisha Burundi huko Ubelgiji alipopewa tunzo na Mfalme Albert wa II kwa juhudi zake za kuboresha maridhiano baina raia warundi waishio nchini humo, alikuwa wakati huu mshauri kwenye ikulu ya rais anaehusika na maswala ya kisiasa na ya kidiplomasia. Alipewa hata majukumu ya kuongoza Jopokazi ya uundaji wa Tume ya ukweli na maridhiano.

Bii Clotilde Nizigama ameendelea kuongoza wizara ya fedha ambayo imeongezwa majukumu ya mipango ya serekali

Martin Nivyabandi, waziri wa zamani wa utawala bora amekabidhiwa wizara ya maendeleo ya tarafa, hapa améchukua nafasi ya Bw. Jean Mupira ambae ameng’atuliwa serekalini.

Bii Clotilde Niragira, waziri wa zamani wa sheria, ambae kutokana na wadadisi wa mambo ni miongoni mwa washauri wakuu wa rais wa Jamhuri, amerejea kwenye baraza la mawaziri kwa kukabidhiwa wizara ya mshikamano wa kitaifa, haki za binadamu na jinsia. Amechukuwa nafasi ya Bii Immaculée Nahayo ambae wakati huu afya yake si ya kuridhisha.

Bw.Pascal Barandagiye, aliewahi kuwa kiongozi wa zamani wa baraza kuu la majaji ni mpya kwenye baraza la mawaziri, amepewa wizara ya sheria akichukuwa nafasi ya Bii Ancilla Ntakaburimvo, ambae katika mwaka moja akiongoza wizara hio alijikuta akikabiliana na matatizo chungu nzima pakiwemo mawakili kutiwa korokoroni, na migomo ya majaji.

Mabadiliko mengine ni upande wa wizara ya nishati na madini ambayo hatamu za uongozi zimekabidhiwa Bw. Côme Manirakiza ambae amechukuwa nafasi ya Bw. Moïse Bucumi.

Waziri huyo ambae ni miongoni mwa vigogo wa utawala, amepewa wizara ya uchukuzi na kazi za serekali akichukuwa nafasi ya Saïd Kibeya.

A nos chers lecteurs

Nous sommes heureux que vous soyez si nombreux à nous suivre sur le web. Nous avons fait le choix de mettre en accès gratuit une grande partie de nos contenus, mais une information rigoureuse, vérifiée et de qualité n'est pas gratuite. Nous avons besoin de votre soutien pour continuer à vous proposer un journalisme ouvert, pluraliste et indépendant.

Chaque contribution, grande ou petite, permet de nous assurer notre avenir à long terme.

Soutenez Iwacu à partir de seulement 1 euro ou 1 dollar, cela ne prend qu'une minute. Vous pouvez aussi devenir membre du Club des amis d'Iwacu, ce qui vous ouvre un accès illimité à toutes nos archives ainsi qu'à notre magazine dès sa parution au Burundi.

Editorial de la semaine

Que la compétition politique soit ouverte

Il y a deux mois, Iwacu a réalisé une analyse de l’ambiance politique avant les élections de 2020 et celles à venir en 2025. Il apparaît que la voix de l’opposition est presque éteinte. Il n’y a vraiment pas de (…)

Online Users

Total 1 479 users online