Kwa mujibu wa duru za kuaminika kutoka familia za wafiwa wakati wa mazishi kwenye makaburi ya Mpanda, askari kutoka Burundi waliyoyapoteza maisha katika mapigano yanayoendeleya huko kijijini Dayniile kwenye umbali wa kilomita 18 kutoka mji mkuu Mogadishu, ni zaidi ya 50. Wengine haijulikane mahala walipo, zasema duru hizo.
<doc1789|left>« Marafiki zetu waliteketea huko Mogadishu, ijuma nne tuliwazika askari 3, asubuhi yake kulihesabiwa jeneza 17 na kesho yake kutazikwa wenginena pengine hadi ijuma pili zoezi hilo litaendelea », alinongoneza kwa hasira moja kati ya askari aliyekuwa akilibeba na wenzake jeneza. Hata sauti ilikuwa ikitoka kwa shida, kawaida askari hua hawapendi kusema mambo yanayowahusu, kwa kila swali, jibu linalotolewa ni ’’nenda kamuulize msemaji’’, walakin mwiko huo aliuvunja siku hio. Hali ilikuwa nzito hata upande wa askari wenzake nyuso zilikuwa za huzuni licha ya kua baadhi yao wanatazamiwa kujielekeza huko Somalia kujiunga na vikosi vya kulinda amani nchini humo chini ya usimamizi wa Umoja wa Afrika. Hapo wiki jana walihitimisha mazoezo maalum ya kijeshi.
Misa ya kuwarehemu na kuwaombea askari hao waliyouwawa huko Somalia katika mchakato wa kurejesha amani nchini humo ilifanyika katika kambi ya kijeshi iitwao ’’DCA’’ kando ya uanja wa ndege wa Bujumbura. Wanahabari hawakuruhusiwa kuingia kwenye ibada hio, kilichosikika ni tarumbeta maalumu iliyohitimisha misa hio. Hata familia zilijulishwa maafa hayo usiku wa kuamkia mazishi hayo. Brigadier general Diomède Ndegeya, Naibu Mkuu wa majeshi alishiriki ibada hio ya misa.
Jeneza zilionekana zikifunikwa bendera ya taifa na ziliwasili huko makaburini Mpanda kutoka kambini zikibebwa kwenye lori za rangi nyeupe za vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika. Kila lori ilikuwa na jeneza nne na ilibidi kufanyike awamu 2 na kulionekana mlolongo wa agari usiokuwa wa kawaida. Kila jeneza ilikuwa ikibebwa na askari huku mbele kukitangulia askari mwengine mwenye msalaba wa rangi nyeusi. Jeneza hizo zilikuwa zikipitishwa katikati ya mistari 2 ya askari wenye kusimama imara na bunduki zao kama ishara ya heshima kwa wanajeshi hao waliopoteza maisha huko Somalia.
Ibada zihusuzo musiba huo huko makaburini Mpanda zilionekana kufupishwa, si jambo la kawaida. Majonzi yalikuwa ni mengi hasa upande wa wajane. Nyimbo za kidini ziliimbwa kwa sauti kubwa na ya huzuni hasa wakati wa viitikio ili waliokuwa wakilia wasisisike sana. Brigadier general Diomède Ndegeya, Naibu Mkuu wa majeshi ailionekana akipiga saluti mbele ya kila kaburi za wahanga hao waliopoteza maisha huko Somalia katika mchakato wa kurejesha amani nchini humo.
« Hatuwezi kuisaliti Somalia kwa kuyaondoa majeshi yetu nchini humo »
<doc1790|right>Kwa mujibu wa kanali Gaspard Baratuza, msemaji wa jeshi la Burundi, idadi ya askari waliouwawa nchini huma haiwezi kua chanzo cha kuyaondoa majeshi ya Burundi Somalia. « Kukubali kushiriki mchakato wa kusaka amani nchini humo, lengo si kutafuta mishahara minono kama wanavyosema watu wenye fikra finyu », anasema kanali Baratuza akikiri kua mapigano yanazidi kupamba moto huko Somalia na kua ni makali. « Lengo ni kuwaondoa wapiganaji wa kundi la Al Shabab kwenye ngome zao za huko Dayniile kwenye umbali wa kilomita karibu 10 kaskazini magharibi mwa mji wa Mogadishuna majeshi ya Umoja wa Afrika pakiwemo askari kutoka Burundi, yako imara », anabaini hayo msemaji wa jeshi la Burundi huku akizidi kukanusha kua katika mapigano yaliyozuka tangu wiki jana kuliuawa askari kutoka Burundi zaidi ya 70.
« Burundi ilikubali kuyatuma majeshi yake huko Somalia katika mchakato wa Umoja wa Afrika wa kurejesha amani nchini humo sababu iliwahi kujinufaisha na kusaidiwa na Jumuia ya kimataifa na hali ya nchi zingine kusita kuvituma vikosi nchini Somalia ni kwa sababu zao », anasema kanali Baratuza. Anahakikisha kua wakatu huu mj mkuu wa Mogadishi unadhibitiwa na majeshi ya serekali ya mpito ya Somalia kwa ushirikiano na vikosi kutoa Uganda na Burundi.
« Katika operesheni hio Burundi ilituma wanajeshi wapatao 4,250 na kila askari anapewa dola za kimarekani 1,028 kwa mwezi na serekali ya Burundi inachukuwa kwa kila mshahara dola zipatazo 200. Zana zinazotumiwa ni kama za kukodiwa na pesa hizo ni za kulipa vifaa hivyo », anabaini hayo msemaji wa Jeshi la Burundi, kanali Gaspard Baratuza. Anakiri kua Burundi haiwezi kuyaondowa majeshi yake nchini Somalia bila nchi hio kupata amani. Anatoleya wito nchi za bara la Afrika akizitaka kuunga mkono juhudi hizo kwa kuvituma vikosi kuchangia katika mchakato wa kurejesha amani nchini Somalia.